Simba Sports Club
News

Onyango arejea kundini, afanya mazoezi na wenzake

12 Sep 2022

Onyango ambae amekosekana kwenye mechi kadhaa atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaosafiri kuelekea Mbeya tayari kwa mchezo wa Jumatano dhidi ya Prisons.

Leo jioni katika Uwanja wetu wa mazoezi wa Mo Arena Bunju, Onyango amejumuika na wenzie kwenye mazoezi yaliyoongozwa na Kocha mkuu wa muda Juma Mgunda.

Advertisement

Onyango anaungana na Henock Inonga, Mohamed Ouattara na Kennedy Juma kuunda safu yetu ya walinzi wa kati.

Back to homepage
Share this story