Omari ni mchezaji kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi tofauti Uwanjani.
Omari anaweza kucheza kwa ufasaha namba 8, 10, 11 na 7 na hicho ni moja ya kitu ambacho kimetuvutia kwake na kuamua kumsajili.
Advertisement
Omari ni kijana mwenye kipaji kikubwa na tunaamini uwezo wake utasaidia timu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25.
Mipango ya klabu ni kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa huku tukizingatia umri kwakuwa tunajenga timu imara ya muda mrefu.