Simba Sports Club
News

Okrah atupia tukipata sare na Ismailia

17 Jul 2022

Mchezo huo wa kirafiki ambao ulikuwa wa kuvutia huku timu zote zikionyesha uwezo mkubwa umepigwa katika Uwanja wa Ismailia saa 11:00 jioni kwa saa Misri ambapo huko nyumbani ni saa 12:00 Jioni.

Mechi hiyo ilikuwa ya mazoezi (Training match) ambayo ni pendekezo la Mwalimu Zoran Maki kuendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi.

Kikosi chetu kilichoanza leo ni

Beno Kakolanga

Shomari Kapombe

Gadiel Michael

Erasto Nyoni

Joash Onyango

Advertisement

Jonas Mkude

Augustine Okrah

Cleutus Chama

Habib Kyombo

John Bocco

Pape Sakho

Kocha Zoran alifanya mabadiliko ya kuwatoa Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Clatous Chama, Habib Kyombo, John Bocco na Pape Sakho na kuwaingiza Ally Salim, Israel Patrick, Victor Akpan, Medie Kagere, Chris Mugalu na Jimmyson Mwanuke.

Back to homepage
Share this story