Simba Sports Club
News

Okrah atupia tukipata sare na Ismailia

17 Jul 2022 By simbasc 1,883 views
Kiungo mshambuliaji Augustine Okrah amefungua akaunti ya mabao baada ya kutupia katika mchezo wa kirafiki wa kimazoezi dhidi ya Ismailia inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri na kumalizika kwa sare ya bao moja. Mchezo huo wa kirafiki ambao ulikuwa wa kuvutia huku timu zote zikionyesha uwezo mkubwa umepigwa katika Uwanja wa Ismailia saa 11:00 jioni kwa saa Misri ambapo huko nyumbani ni saa 12:00 Jioni. Mechi hiyo ilikuwa ya mazoezi (Training match) ambayo ni pendekezo la Mwalimu Zoran Maki kuendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi. Kikosi chetu kilichoanza leo ni Beno Kakolanga Shomari Kapombe Gadiel Michael Erasto Nyoni Joash Onyango Jonas Mkude Augustine Okrah Cleutus Chama Habib Kyombo John Bocco Pape Sakho Kocha Zoran alifanya mabadiliko ya kuwatoa Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Clatous Chama, Habib Kyombo, John Bocco na Pape Sakho na kuwaingiza Ally Salim, Israel Patrick, Victor Akpan, Medie Kagere, Chris Mugalu na Jimmyson Mwanuke.
Advertisement
Back to homepage
Share this story