Wachezaji wetu tisa wameziwakilisha nchi zao katika mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kwa nchi za Afrika kutafuta nafasi hiyo zilizopigwa jana.
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilikuwa na kibarua dhidi ya Benin katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa huku wachezaji wetu watano wakianza moja kwa moja kikosi cha kwanza.
Mlinda mlango Aishi Manula alisimama langoni huku walinzi Israel Patrick na Mohamed Hussein wakianza pembeni Mzamiru Yassin akiwa idara ya kiungo wa ulinzi huku nahodha John Bocco akiongoza mashambulizi.
Mshambuliaji Kibu Denis aliingia dakika ya 45 kipindi cha pili na kuonyesha uhai katika idara ya ushambuliaji ya Stars ingawa hakufanikiwa kufunga.
Mchezo mwingine ulikuwa kati ya majirani Uganda na Rwanda ambapo kiungo wetu Taddeo Lwanga alianza kwenye kikosi cha (The Cranes) huku mshambuliaji Medie Kagere akiongoza mashambulizi ya (Amavubi).
Mlinzi wetu wa kati Joash Onyango alianza kwenye kikosi cha Kenya (Harambee Stars) kilichoikabili Mali na kukamilisha idadi ya wachezaji nane.
LeoTimu ya Taifa ya Malawi (The Flames) itashuka dimbani kuikabili Ivory Coast huku tukitarajia kuwaona nyota wetu Peter Banda na Duncan Nyoni wakianza