Simba Sports Club
News

Nyota watakaotuwakilisha dhidi ya Yanga leo

30 Apr 2022 By simbasc 1,113 views

Mshambuliaji Chris Mugalu ataongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa leo Aprili 30, saa 11 jioni.

Mugalu atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo watatu washambuliaji Clatous Chama, Bernard Morrison na Pape Sakho.

Katika eneo la kiungo wa ulinzi kama kawaida wamepangwa Jonas Mkude na Sadio Kanoute.

Joash Onyango na Henock Inonga wataongoza idara ya ulinzi wakati Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wakicheza pembeni.

Advertisement

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga( 29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7), Clatous Chama (17), Bernard Morrison (3)

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Rally Bwalya (8), John Bocco (22),
Kibu Denis (38), Yusuf Mhilu (27).

Back to homepage
Share this story