Uongozi wa klabu umewashukuru wachezaji watatu wa kimataifa waliokuja kufanya majaribio kwenye kikosi chetu katika mashindano ya Mapinduzi ingawa hakuna aliyepata nafasi ya kusajiliwa.
Wachezaji wote watatu wameonyesha uwezo mkubwa na pia wamechangia kupatikana kwa ubingwa wa Mapinduzi 2022.
Nyota hao ni Sharaf Eldin Shiboub (Sudan), Check Moukoro (Ivory Coast) na David Udoh (Nigeria) ambao wote walipata nafasi ya kucheza.
Advertisement
Kukosa nafasi ya kusajiliwa kwenye kikosi chetu haimaanishi viwango vyao viko chini bali ufinyu wa idadi ya wachezaji wa Kimataifa wanaohitajika kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa.
Uongozi unaamini wachezaji hao watasajiliwa na timu nyingine kutokana na uwezo mzuri walioonyesha.