Simba Sports Club
News

Nyota tisa waitwa Taifa Stars

19 Aug 2022 By simbasc 1,139 views
Wachezaji tisa kutoka kwenye kikosi chetu wameitwa katika Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayojiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Uganda. Baada ya kuonyesha kiwango safi katika mechi za maandalizi ya msimu (Pre Season) mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya naye amejuimuishwa kikosini. Kiungo mkabaji Jonas Mkude na mshambuliaji mpya Habib Kyombo nao ni miongoni mwa nyota 25 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwa ajili ya mechi hizo. Wachezaji hao walioitwa ni walinda mlango Aishi Manula Beno Kakolanya walinzi Shomari Kapombe Mohamed Hussein Kennedy Juma Viungo Jonas Mkude Mzamiru Yassin Washambuliaji Kibu Denis Habib Kyombo Stars itaingia kambini Jumapili na mchezo wa kwanza utapigwa Agosti 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa na marudio itakuwa Septemba 3 jijini Kampala, Uganda.
Advertisement
Back to homepage
Share this story