Wachezaji hao ni walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' na Henock Inonga.
Wengine ni viungo Mzamiru Yassin, Clatous Chama na Saido Ntibazonkiza.
Kuingiza wachezaji wengi kuliko timu yoyote kwenye kikosi bora cha Ligi cha msimu ni wazi kwamba tumekuwa na timu bora ingawa hatufanikiwa kuchukua ubingwa.
Advertisement
Katika msimu wa 2022/23 sisi ndio tumefunga mabao mengi na kuruhusu machache.
Katika msimu wa 2022/23 sisi ndio timu iliyofunga mabao matatu kwenye mechi moja (hat trick) nyingi kuliko yoyote.