Simba Sports Club
News

Nyota Simba Queens afunguka kuelekea msimu mpya

20 Dec 2021 By simbasc 1,334 views

Kiungo mshambuliaji wa Simba Queens, Joelle Bukulu amefunguka kuwa maandalizi kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women's Premier League) yanaendelea vizuri na tupo tayari kutetea taji letu.

Simba Queens imepangwa kuanza kutetea ubingwa wa ligi kwa kucheza dhidi ya Ruvuma Queens mchezo utakaopigwa Desemba, 23 katika Uwanja wa Mo Simba Arena.

Bukulu amesema anaamini msimu utakuwa mgumu kutokana na timu nyingi kujiandaa vizuri lakini nasi tutahakikisha tunapambana kutetea ubingwa.

Advertisement

"Msimu utakuwa mgumu kwa sababu timu zote zimejipanga ili kufanya vizuri, sisi kama mabingwa tutapambana kuhakikisha tunatwaa tena taji hili ingawa tunajua haitakuwa kazi rahisi.

"Kuelekea mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Ruvuma maandalizi yanaendelea vizuri, wachezaji tupo kwenye hali nzuri tunatarajia mechi ya ushindani lakini tumejipanga kushinda," amesema Bukulu.

Back to homepage
Share this story