Simba Sports Club
News

Nyota 20 watakaosafiri kuifuata Jwaneng Botswana

30 Nov 2023 By simbasc 870 views
Kikosi chetu kitaondoka kesho alfajiri kuelekea Botswana tayari kwa ajili ya mchezo wa pili hatua ya makundi dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja Obedi Itani Chilume uliopo katika Mji wa Francistown. Kikosi kitaondoka na wachezaji 20 ambao tunaamini wataweza kutupatia matokeo chanya katika mchezo huo ambao tunafahamu utakuwa mgumu. Kikosi kamili kitakachosafiri Makipa: Ayoub Lakred, Hussein Abel na Ally Salim Walinzi: Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Malone Fondoh, Henock Inonga, Kennedy Juma, Israel Mwenda na Hussein Kazi Viungo: Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Dennis Kibu, Saidi Ntibazonkiza, Luis Miquissone na Essomba Onana Washambuliaji : Jean Baleke na Moses Phiri
Advertisement
Back to homepage
Share this story