Nyota hao ni wale ambao usajili wao umekamilika pamoja na kupata vibali vya safari huku wakiongezwa wengine kutoka timu ya vijana.
Wachezaji wote ambao tumetangaza kuwasajili wiki iliyopita ni miongoni mwa nyota waliopo safarini.
Wachezaji hao ni Morice Abraham, Hussein Semfuko, Allasane Kante, Jonathan Sowah, Mohamed Bajaber, Mzamiru Yassin, Salehe kikuya na Kibu Denis.
Advertisement
Kutoka timu ya vijana waliosafiri ni Bashir Salum, Ally Mbegu na Alexander Erasto.
Wachezaji hao wanatarajiwa kuwasili nchini Misri na kujiunga na wenzao mchana wa leo.