Simba Sports Club
News

Ntibazonkiza: Nimefurahi kuwapa furaha Wanasimba

1 Jan 2023

Ntibazonkiza amesema anajisikia furaha kuanza vizuri katika kikosi chetu na anaamini ataendelea kufanya hivyo kutokana na ushirikano anaopewa na wachezaji wenzake.

Akizungumzia alivyoshangilia bao lake la pili amesema alikwenda kushangilia mbele ya kamera kwa kuwa alikuwa anamtumia ujumbe binti yake ambaye alikuwa anamtazama kupitia luninga.

Advertisement

"Ni furaha kwangu kuisaidia timu yangu kupata ushindi na kuwapa furaha Wanasimba, nitaendelea kujituma kuhakikisha naendelea kuisaidia timu.

"Bao la pili nilishangilia kwenye kamera kwa ajili ya kumtumia ujumbe binti yangu na kumwambia nampenda kwa kuwa nilikuwa najua ananitazama," amesema Ntibazonkiza.

Back to homepage
Share this story