Simba Sports Club
News

Ntibazonkiza Mchezaji bora wa Mashabiki Mwezi Mei

12 Jun 2023

Ntibazonkiza amewashinda walinzi Shomari Kapombe na Henock Inonga ambao ameingia nao fainali ya kinyang'anyiro hicho.

Katika mwezi Mei Ntibazonkiza amecheza dakika 450 akifunga mabao saba na kusaidia kupatikana kwa mengine matano.

Mchanguo wa kura zilivyopigwa

Kura Asilimia Nafasi

Inonga 68 5.57 3

Advertisement

Ntibazonkiza 1021 83.62 1

Kapombe 132 10.81 2

Ntibazonkiza atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

Hii ni mara ya pili kwa Ntibazonkiza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi baada ya kufanya hivyo Januari mwaka huu.

Back to homepage
Share this story