Saido alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 3.
Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema Saido anaendelea vizuri na kilichomfanya kutokuwepo kwenye kikosi kinachosafiri ni kutokana na kutofanya mazoezi pamoja na wenzake.
Dk. Edwin ameongeza kuwa Saido yupo chini ya uangalizi na ataungana na kikosi kitakaporejea nyumbani kutoka Guinea.
"Saido alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars, hali yake imeimarika lakini hawezi kusafiri kwa kuwa hayuko timamu na hajafanya mazoezi na wenzake. Timu ikirejea atajiunga na wenzake," amesema Dk. Edwin.
Wachezaji wengine waliobaki kutokana na kutokuwa katika mpango wa mchezo ni Jonas Mkude, Peter Banda na Jimmyson Mwanuke.