Ngoma alifunga bao la tatu kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Ladaki Chasambi dakika ya 54 katika ushindi huo wa mabao 5-2 na ndipo aiposhangilia kwa kuonyesha ishara ya vidole vitano
Ngoma amsema wakati timu inaenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko alisimama mbele ya jukwaa kuu na kuwaeleza viongozi kuwa mechi itamalizika kwa ushindi wa mabao matano.
“Wala sikuwa na wasiwasi wowote wakati natoa ahadi hiyo kutokana na mambo matatu makubwa kwanza siku moja kabla ya mechi kwenye uwanja wa mazoezi wachezaji wenzangu haswa wanaocheza kwenye eneo la kushambulia walifanya vizuri na mara kwa mara walikuwa wanafunga mabao."
“Jambo la pili tulikubaliana na wachezaji wanzangu kuwa tunatakiwa kushinda mechi ngumu haswa hizi za ugenini ambazo zilitusumbua msimu uliopita na jambo la mwisho ni morali kubwa kwa wachezaji wote tuliyokuwa nayo kila mmoja alikuwa anatamani kuona tunashinda mabao mengi," amesema Ngoma.
Baadhi ya Viongozi waliokuwa wamekaa jukwaa kuu na kushuhudia ahadi iliyotolewa na Ngoma ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Hussein Kitta, Mratibu, Abbas Ally na Maneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally.