Simba Sports Club
News

Nangu kufanyiwa upasuaji, Yakoub mbioni kurejea uwanjani

12 Feb 2026

Ahmed amesema Nangu alipata majeraha ya kifundo cha mguu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ES Tunis uliopigwa Uwanja wa Benjamin, Februari Mosi ambapo kwa mujibu wa madaktari matibabu yake lazima afanyiwe upasuaji.

Kuhusu mlinda mlango, Yakoub Suleiman ambaye alipata majeraha akiwa na kikosi cha Tanzania kwenye michuano ya AFCON nchini Morocco nae anaendelea vizuri na yuko mbioni kurejea uwanjani.

Advertisement

"Wachezaji wetu wanaendelea vizuri isipokuwa Nangu ambaye taarifa ni kwamba mwishoni mwa wiki tutampeleka Afrika Kusini kwa ajili ya kwenda kufanyiwa upasuaji, ameumia kifundo cha mguu."

"Baada ya upasuaji kukamilika tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusema atakuwa nje kwa muda gani, kwa upande wa Yakubu Suleiman maendeleo ni mazuri na muda wowote atarejea kikosini," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story