Nangu alipata majeraha ya kifundo cha mguu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ES Tunis uliopigwa Uwanja wa Benjamin, Februari Mosi ambapo kwa mujibu wa madaktari matibabu yake ilikuwa lazima afanyiwe upasuaji.
Baada ya upasuaji huo Nangu ameushukuru Uongozi wa klabu kwa kufanikisha matibabu hayo ambayo anategemea yatamaliza kabisa tatizo lake na atarejea uwanjani akiwa na nguvu zaidi.
Advertisement
"Naushukuru Uongozi wa klabu yangu ya Simba kwa kufanikisha upasuaji huu, ninaamini baada ya hapa nitapona na kurejea kwenye majukumu yangu," amesema Nangu.
Kwa mujibu wa taarifa ya daktari Nangu anatakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi sita ili kuuguza jeraha hilo.