Simba Sports Club
News

Namba za jezi watakazotumia nyota wapya

21 Jan 2023

Uchaguaji wa jezi umezingatia Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwa zile ambazo zimewahi kutumiwa hata kama wachezaji wameondoka kikosini bado zimesajiliwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) na majina yao yanaonekana.

SAWADOGO JEZI NAMBA 3

Kiungo mkabaji Ismael Sawadogo tuliyemsajili kutoka Difaa El Jadida atavaa jezi namba 3 ambayo tangu kuanza kwa msimu huu haikuwa na mchezaji aliyekuwa anaitumia.

Msimu uliopita jezi hiyo ilikuwa inavaliwa na Bernard Morrison ambaye ameondoka.

Hata hivyo mwenyewe Sawadogo alikuwa anapenda kutumia jezi namba 2 ambayo tayari inatumiwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael.

BALEKE JEZI NAMBA 4

Mshambuliaji Jean Othos Baleke ambaye tumemsajili kutoka TP Mazembe atavaa jezi namba 4.

Advertisement

Jezi hiyo msimu uliopita ilikuwa inavaliwa na kiungo mkabaji Taddeo Lwanga ambaye ameondoka.

Wakati akiwa Mazembe Baleke alikuwa anavaa jezi namba 12 ambayo kwa sasa inatumiwa na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

MOHAMED MUSSA JEZI NAMBA 14

Mshambuliaji chipukizi ambaye tumemsajili kutoka Malindi ya Zanzibar yeye atavaa jezi namba 14.

Jezi hiyo msimu uliopita ilikuwa inavaliwa na mshambuliaji, Meddie Kagere.

Wachezaji wote watatu ni miongoni mwa nyota 19 waliopo Dodoma tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji na watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani.

Back to homepage
Share this story