Simba Sports Club
News

Mzizima Derby kupigwa Zanzibar Septemba 26

21 Sep 2024

Mchezo huo ulikuwa Haujapangiwa ratiba kutokana na ushiriki wa michuano ya Afrika kwa timu zote lakini sasa ni rasmi utapigwa Visiwani Zanzibar.

Maandalizi ya mchezo huo ambao ni muhimu kwetu yataanza mara tu tutakapomaliza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli utakaopigwa kesho.

Advertisement

Mchezo huo utakuwa ni wa tatu kwetu baada ya kushinda mechi mbili za kwanza dhidi ya Tabora United na Singida Fountain Gate.

Back to homepage
Share this story