Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin, amewaomba mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Manungu huku akiwaahidi furaha baada ya mechi.
Mzamiru amesema mchezo utakuwa mgumu lakini si sana na kutokana na maandalizi tuliyofanya anaamini tutaibuka na ushindi kesho.
Kiungo huyo ameongeza kuwa anajisikia furaha kila anapocheza mkoani Morogoro sababu ndiyo nyumbani kwao pia mazingira ni mazuri.
Advertisement
"Ninachowaomba mashabiki zetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kesho, hii ndiyo timu yao. Tunachowaahidi ni furaha wao waje nasi tutashinda uwanjani.
"Morogoro ni nyumbani, nafurahi sana kucheza huku, mazingira ni mazuri ambayo yanatuwezesha kufanya kila kitu," amesema Mzamiru.