Simba Sports Club
News

Mwana FA: Simba nchi ipo nyuma yenu Jumamosi

22 Nov 2023

Mwana FA ameyasema hayo alipotembelea mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena ambapo ameweka wazi hana wasiwasi na ubora wa kikosi na anaamini tunaweza kupata ushindi Jumamosi.

Mwana FA ameongeza kuwa katika mpira kuna kipindi unapata matokeo ambayo hakufurahishi lakini unatakiwa kusonga mbele na kusahau ya nyuma.

"Binafsi sina wasiwasi na uwezo wenu, mimi nawajua mpaka kwa majina yenu. Kinachotakiwa ni kuhakikisha mnajitoa kuhakikisha tunapata ushindi Jumamosi.

Advertisement

"Kama kuna jambo kwa upande wetu Serikali tunatakiwa kufanya basi tutafanya ili kila kitu kiende sawa, wajibu wenu ni kutupa furaha Jumamosi kwa ushindi dhidi ya ASEC," amesema Mwana FA.

Mwana FA amewakumbusha wachezaji kuwa milioni 10 inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kila goli linalofungwa ipo pale pale na 'Mzigo' utakabidhiwa kwa nahodha baada ya mechi tu kumalizika.

Back to homepage
Share this story