Mugalu aliumia katika mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza wakati Dilunga aliumia mazoezini wakati timu inajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas Jumanne iliyopita.
Daktari wa timu, Edwin Anakret amesema baada ya wiki mbili Mugalu ataanza mazoezi pamoja na wenzake wakati Dilunga atasubiri vipimo tena kabla ya kuruhusiwa kurudi uwanjani rasmi.
Advertisement
Dk. Anakret amesema pamoja na mambo mengine nyota hao wanaendelea vizuri na wangeweza kurudi uwanjani hata kabla ya siku hizo zilizotajwa lakini wataendelea kuwa chini ya uangalizi hadi wakapokuwa fiti kabisa.