Simba Sports Club
News

Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Yanga Leo

28 May 2022

Mugalu atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji wawili Kibu Denis na Pape Sakho ambao watatokea pembeni.

Katika eneo la kiungo wa kati kocha Pablo Franco amewapanga viungo watatu Taddeo Lwanga, Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

Mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya atasimama katika milingoti mitatu akichukua nafasi ya Aishi Manula ambaye ameumia vidole viwili vya mkono.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Advertisement

Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Taddeo Lwanga (4), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Aishi Manula (28), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27).

Back to homepage
Share this story