Simba Sports Club
News

Mugalu, Kibu warejea uwanjani

3 Mar 2022

Washambuliaji Chris Mugalu na Kibu Denis wameanza mazoezi baada ya kupona majeraha yaliyowafanya kukaa nje ya uwanja kwa muda sasa.

Hata hivyo wawili hao wanafanya mazoezi chini ya uangalizi maalumu wa madaktari kabla ya kuruhusiwa kuungana rasmi na wenzao.

Kibu ambaye anashika nafasi ya pili ya ufungaji ndani ya kikosi hajaonekana uwanjani kwa muda sasa lakini tayari amepona na utimamu wake wa mwili ukitengamaa ataanza kushuka dimbani.

Advertisement

Kwa upande wake kiungo mkabaji Mzamiru Yassin naye amejiunga na kikosi kujiandaa na mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Biashara United utakaopigwa kesho saa moja usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kumaliza masuala yake ya kifamilia.

Rally Bwalya pia amejiunga na timu baada ya kurejea kutoka kwao nchini Zambia alipokuwa akishughulikia masuala ya kifamilia.

Back to homepage
Share this story