Simba Sports Club
News

Mugalu, Kanoute warejea mazoezini fiti kuwavaa Pamba

13 May 2022

Mugalu na Kanoute walipata majeraha hayo katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga uliopigwa Aprili, 30 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wawili hao wamefanya mazoezi ya mwisho pamoja na wenzao kujiandaa na mchezo wa kesho wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Pamba utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mugalu na Kanoute wanaungana na Taddeo Lwanga ambaye naye alikuwa majeruhi na tayari amerejea na kujiunga na wenzake.

Advertisement

Kurejea kwa Kanoute na Taddeo kunalipa ahueni benchi la ufundi kutokana na idadi ya viungo wakabaji kupata majeraha ambapo alibaki Mzamiru Yassin pekee aliyekuwa fiti.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar kocha, Pablo Franco aliamua kumtumia, Henock Inonga katika eneo la kiungo wa ulinzi pamoja na Mzamiru.

Back to homepage
Share this story