Ahmed ameyasema hayo katika siku ya pili ya hamasa kuelekea mchezo huo katika viwanja vya Ukonga Mazizini ambayo lengo lake ni kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu.
Ahmed ameweka wazi kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunavuka na kuingia nusu fainali na kuweka wazi kuwa kuna watu ambao hawataki kutuona tukifanikiwa na ndio sababu ya kumualika Mtume Mwamposa.
"Safari hii tumedhamiria ubaya ubwela na tunamualika kila mtu mwenye mchango mkubwa katika jamii. Wachawi ni wengi ndugu zangu, kuna watu wamekunja nafsi kwelikweli. Kwa mantiki hiyo namtamgaza mgeni mwingine Maalum ambaye ni Mtumishi wa Mungu Mtume Boniface Mwamposa 'Buldozer' ambaye tutakuwa nae siku ya Jumatano," amesema Ahmed.
Mtume Mwamposa anaungana na Viongozi wengine kama Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Wallace Karia ambao tayari tumewaalika kwenye mchezo wetu wa Jumatano.