Simba Sports Club
News

Moussa Camara ni Mnyama

2 Aug 2024

Camara raia wa Guinea mwenye umri wa miaka 25 amekuja kuongeza nguvu katika idara ya golikipa kwakuwa tunahitaji kufanya vizuri msimu ujao.

Baada ya kusaini mkataba Camara amesema ana ushukuru Uongozi wa klabu kwa kumpa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi chetu.

Camara amesema Simba ni timu kubwa na wachezaji wengi Afrika wana ndoto ya kuichezea kama ilivyo yeye kwake ni heshima kubwa.

Advertisement

"Namshukuru Mungu kuwa hapa, pia nawashukuru Viongozi wa Simba kunipa nafasi na kuniamini kuwa naweza kuwa sehemu ya timu hii."

"Nipo hapa kwa ajili ya kuhakikisha naisadia timu kufanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu," amesema Camara.

Back to homepage
Share this story