Simba Sports Club
News

Morrison, Mkude, Kagere wachuana Mchezaji Bora Novemba

29 Nov 2021 By simbasc 4,705 views

Nyota wetu watatu Bernard Morrison, Jonas Mkude na Medie Kagere wameingia fainali ya kinyang'anyiro cha Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Kuchaguliwa kwa wachezaji hao kumetokana na uwezo mkubwa walioonyesha katika mechi tulizocheza Novemba.

Awali walikuwa wachezaji watano akiwamo walinzi Joash Onyango na Mohamed Hussein lakini wamechujwa na Kamati Maalumu na kubaki watatu ambao watakaopigiwa kura na mashabiki kupitia tovuti rasmi ya klabu ya www.simbasc.co.tz

Advertisement

Zoezi la kupiga kura limefunguliwa leo na litafungwa Desemba Mosi saa 10 jioni ambapo atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.

Hassan Dilunga aliibuka mshindi wa mwezi Oktoba na kujinyakulia kitita cha Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini wa tuzo Emirate Aluminium ACP.

[totalpoll id="6567"]
Back to homepage
Share this story