Simba Sports Club
News

Morrison, Miquissone, Bocco mchuano mkali Tuzo ya Mchezaji Bora

28 Jun 2021 By simbasc 11,415 views

Nyota watatu Bernard Morrison, Luis Miquissone na John Bocco wameingia fainali ya kumsaka Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Juni (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Kabla ya mchujo wa Kamati Maalumu ya tuzo hizo,  nyota hao walikuwa watano akiwamo Rally Bwalya na Pascal Wawa.

Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa mshabiki inadhaminiwa na Kampuni ya Emirate Aluminum Profile ambayo ilianza kutolewa Februari mwaka huu.

Advertisement

Mshindi kati ya nyota hao watatu ni yule atakayepata kura nyingi zitakazopigwa na mashabiki kupitia tovuti hii rasmi ya klabu.

Zoezi la kupiga kura litaanza leo usiku na litakamilika Julai 1 Mosi usiku na mshindi atakayetangazwa atajinyakulia kitita cha Sh 1,000,000 kutoka Emirate Aluminum Profile.

[totalpoll id="4952"]
Back to homepage
Share this story