Simba Sports Club
News

Morrison aruhusiwa kurejea kikosini

14 Feb 2022

Morrison alituhumiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu ambapo alisimamishwa kwa muda pamoja na kutakiwa kutoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez.

Morrison aliomba radhi kwa uongozi na benchi la ufundi na mapema leo alifika katika ofisi za klabu na kuzungumza na Barbara.

Katika maelezo yake Morrison aliomba radhi kwa makosa yake na ameahidi kutorudia.

Advertisement

Kwa maslahi mapana ya pande zote mbili Mtendaji Mkuu amemsamehe Morrison na kisha kumruhusu kujiunga na wenzie kikosini.

Tayari Morrison ameshawasili kambini na jioni leo atafanya mazoezi na wenzie katika Uwanja wa Mo Arena uliopo Bunju Jijini Dar Es Salaam.

Back to homepage
Share this story