Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison, ameweka wazi kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ikiwa ni sehemu ya kuomba radhi kwa mashabiki, viongozi na wadhamini kwa matokeo mabaya ya nyuma.
Morrison ambaye alikuwa nyota wa mchezo wa jana dhidi ya Red Arrows, amesema kuendelea kushinda na kucheza soka safi uwanjani itakuwa ni sehemu ya kuomba msaamaha kwa wadau wetu.
"Nichukue nafasi hii kuomba msamaha kwa viongozi, mashabiki na wadhamini kwa matokeo mabaya tuliyopata awali, tunajua waliumia kama tulivyoumia sisi lakini ndiyo soka lilivyo," amesema Morrison.
Katika mchezo wa jana Morrison alihusika katika mabao yote matatu akifunga mawili na kusaidia kupatikana moja (assist) lililofungwa na Medie Kagere baada ya kuwalamba chenga walinzi wa Red Arrows.