Simba Sports Club
News

Morrison afungiwa kwa utovu wa nidhamu

4 Feb 2022

Aidha, kutokana na vitendo hivyo, licha ya uongozi kumsimamisha Morrison kwa muda pia ametakiwa kutoa maelezo ya maandishi ndani ya siku saba na endapo atashindwa kufanya hivyo hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Katika vitendo hivyo, Morrison ametajwa kuwa na tabia endelevu ya kutoka kambini bila ruhusa kinyume na utaratibu.

Advertisement

Mara ya mwisho Morrison alitoka kambini bila ruhusa ambapo uongozi wa benchi la ufundi ulimpa maelekezo kuwa asirejee hadi atakapoonana na Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez.

Hata hivyo, pamoja na maelekezo hayo Morrison hakutiii maagizo na kuendelea kubaki nje ya kambi jambo ambalo uongozi umeonelea si la kufumbiwa macho.

Back to homepage
Share this story