Morocco tumemtangaza jana jioni kuwa kocha wetu mkuu wa muda na tayari amejiunga na timu na ameongoza mazoezi ya kwanza.
Morocco ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' atakiongoza kikosi chetu mpaka tutakapopata kocha mkuu mpya.
Advertisement
Baada ya mazoezi ya leo kikosi kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa keshokutwa Alhamisi.