Abraham amesema morali za wachezaji wote zipo juu na wapo tayari kupambana mpaka mwisho kuhakikisha ushindi unapatikana ugenini.
Abraham amewaomba mashabiki kuendelea kuiunga mkono timu yao licha ya matokeo ya mchezo wa kwanza kutowafurahisha.
Abraham ameongeza kuwa changamoto ya timu kutengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia zinafanyiwa kazi mazoezini na katika mchezo wa Jumapili kutakuwa na mabadiliko makubwa.
Advertisement
"Tangu tumewasili nchini Mali tumekuta hali ya hewa ni kawaida kama ilivyo nyumbani hilo ni jambo chanya kwetu kama wachezaji."
"Tunafahamu itakuwa mechi itakuwa ngumu lakini kama wachezaji tumejipanga kuhakikisha tunapambana mpaka mwisho kuwarejeshea furaha mashabiki wetu," amesema Abraham.