Simba Sports Club
News

Mo: Tunashinda pamoja, Tunafungwa pamoja

19 Feb 2023 By simbasc 172 views
Rais wa Heshima na muwekazaji wa klabu, Mohamed Dewji 'Mo' amesema hatupaswi kukata tamaa baada ya jana kupoteza nyumbani dhidi ya Raja Casablanca. Mo amesema tunatakiwa kuendelea kuwaunga mkono wachezaji wetu na kuwapa sapoti sio kuwavunja mkono. Mo ameongeza kuwa sio mara zote utapata matokeo mazuri kwahiyo tunapaswa kukubaliana na kila hali. "Simba tunafunga pamoja, tunafungwa pamoja. Hatukati tamaa. Tutaendeleza mapambano," amesema Mo. Kikosi kitashuka dimbani Jumanne kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi ya NBC utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Advertisement
Back to homepage
Share this story