Simba Sports Club
News

Mo Simba Arena kukamilika baada ya wiki mbili

1 Nov 2021

Uwanja wetu wa Mo Simba Arena unaendelea na ukarabati kwenye eneo lake la kuchezea (pitch) ambao unatarajia kukamilika wiki mbili kutoka sasa.

Tangu kuanza kwa ukarabati huo kikosi chetu kimekuwa kikifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mashindano mbalimbali.

Advertisement

Ukarabati huo ukikamilika kikosi kitarejea kufanya mazoezi katika uwanja huo ambao una sehemu mbili za kuchezea ile ya nyasi halisi na bandia.

Ujenzi wa Uwanja wa Mo Simba Arena umepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kukodi viwanja kwa ajili ya maandalizi ya michuano mbalimbali.

Back to homepage
Share this story