Mo ameweka wazi msimu ujao tutafanya usajili makini wa wachezaji na kuliongezea ngumu benchi la ufundi lengo likiwa ni kuifanya timu kuwa imara katika mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa.
Mo ameenda mbali zaidi kwa kusema mbali na usajili makini tutaokafanya pia kutakuwa na mabadiliko katika Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimeti ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea.
Aidha Mo amewataka wanachama na wapenzi wa klabu kuacha kutoa maneno yakuvunja umoja badala yake kuwa pamoja katika kipindi hiki cha mpito ili kuweza kufikia malengo yetu.
"Mimi malengo yangu ni yale yake ya kuhakikisha Simba inachukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, tumeweka mipango thabiti ya usajili kuelekea msimu ujao ili kuhakikisha tunakuwa na timu imara," amesema Mo.