Simba Sports Club
News Videos

Mo Dewji: Tunaelekea kwenye malengo yetu makubwa

20 Jan 2025

Mo amesema ushirikiano mkubwa kutoka kwa Bodi ya Wakurugenzi, Menejimeti, Benchi la Ufundi, Wachezaji, Serikali na mashabiki umechangia mafanikio tuliyopata mpaka kufikia sasa.

Mo amesema ndoto kubwa tunaendelea kupambana ili kuzitimiza huku akiwapongeza Viongozi wenzake benchi la ufundi na wachezaji kwa kazi kubwa wanayofanya.

"Mafanikio haya yanatakiwa kuwa chachu ya kuendelea kufanya vizuri ili kufikia malengo makubwa tuliyojiwekea ya kuchukua taji la Afrika."

Advertisement

"Siku zote ndoto haiwezi kuwa mpaka pale itakapokamilika. Tunashukuru pia kwa sapoti ya Serikali kwa 'goli la mama' ambalo limekuwa chachu na hamasa kwa wachezaji pamoja na mashabiki wetu ambao mmekuwa nasi nyakati zote," amesema Mo.

Mo ameongeza kuwa kwa sasa tunaelekeza nguvu kwenye mechi za robo fainali ili kuanza maandalizi mapema kwakuwa tunahitaji kufanya vizuri.

Back to homepage
Share this story