Simba Sports Club
News

Mo awatembelea wachezaji kambini kuwatia moyo

9 Feb 2022

Mo ambaye ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' na Mjumbe wa Bodi, Mulamu Ng'ambi amewataka wachezaji kuhakikisha wanapambana ili tupate ushindi.

"Kila kitu kinawezekana katika mpira kama kila mtu ataongeza jitihada na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

"Mimi binafsi ninawaamini sana, najua mnaweza kufanya makubwa na uongozi uko nyuma yenu. Tumetolewa Ligi ya Mabingwa sasa tuko Shirikisho tupambane tufikie malengo tuliyokuwa tumejiwekea," amesema Mo.

Advertisement

Kwa upande wake Try Again amesema endapo wachezaji watapambana kupigania jezi ya Simba anaamini hakuna atakayetuzuia kufikia malengo tuliyojiwekea katika michuano hiyo.

"Tuna timu bora ambayo inaweza kucheza na yoyote. Kama wachezaji mtaamua kupambana ninaamini hakuna atakayeweza kutuzuia," amesema Try Again

Back to homepage
Share this story