Simba Sports Club
News

Mo awapa mzuka wachezaji kuimaliza Orlando

23 Apr 2022

Mo amezungumza na wachezaji kwa njia ya video na kuwaambia tuna uwezo mkubwa wa kuingia nusu fainali na kuitupa nje Orlando kama kila mmoja atatimiza vema majukumu yake uwanjani.

Amesema Orlando wametudharau kwa kutoa maneno ambayo yanaonyesha hatukustahili kuwafunga kwenye mchezo wa kwanza hivyo tunapaswa kuwathibitishia kuwa sisi ni timu kubwa kwa kuwatupa nje ya mashindano.

Mo ameenda mbali kwa kuwakumbusha tulivyoitoa Zamalek ya Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003 ambapo hakuna aliyeamini kama tunaweza kuwavua ubingwa miamba hiyo ya Afrika.

Advertisement

"Mimi naamini tunaweza kuwafunga Orlando na kutinga nusu fainali. Tunapaswa kuwaonyesha kuwa tulistahili kuwafunga na tunawatoa katika ardhi yao ya nyumbani.

"Labda niwakumbushe mwaka 2003 tuliwafunga Zamalek bao moja nyumbani, tulivyoenda kwao wakatufunga moja tukaenda kwenye penati tukawatoa, kwa hiyo kila kitu kinawezekana. Msijidharau tunaweza kuwatoa Orlando kama tukipambana," amesema Mo.

Back to homepage
Share this story