Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Mohamed Dewji (Mo) leo ametembelea mazoezi ya kikosi chetu katika viwanja vyetu Mo Simba Arena kwa ajili ya kuwapa motisha kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi wiki hii.
Mo ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi kuwapa hamasa wachezaji kujitoa kupigania nembo ya klabu siku ya Jumamosi.
Wachezaji wameonyesha kufurahishwa na uwepo wa 'wakubwa' hao huku wakionekana kuwa tayari kwa ajili ya mchezo ambao huvuta hisia za mashabiki ndani na nje ya nchi.
Kikosi kimeingia rasmi kambini juzi Septemba 21 baada ya kumalizika kwa Tamasha la Simba Day ambalo liliweka rekodi ya kuingiza mashabiki wengi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kama tutafanikiwa kuifunga Yanga na kutwaa Ngao ya Jamii itakuwa ni mara ya tano mfululizo na kuweka rekodi nyingine.