Uhusiano huo utajikita kwenye kufungua fursa kwa vijana chipukizi kupitia timu zetu za vijana, kuimarisha ubora wa Simba ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Akiwa nchini Ujerumani Mo amefanya mazungumzo na Viongozi wa Stuttgart katika kukuza na kuendelea wachezaji kutoka kwenye Akademi yetu pamoja na kushirikiana kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo katika mpira wa miguu.
Advertisement
Mo ameweka wazi dhamira yake ni kuifanya Simba kufanya vizuri sio ndani pekee bali na kimataifa ndio maana amekuwa akikutana na watu mbalimbali kwa ajili ya ushirikiano akianza kwenye kukuza na kuendelea vipaji vya wachezaji.
Mo amesema ukuaji wa klabu yetu unatakiwa kuwanufaisha wachezaji wa Kitanzania pamoja na kuinua hadhi ya soka letu.