Simba Sports Club
News

Mo amuongeza Mpanzu miaka miwili

23 Mar 2026

Mo amekuwa na utaratibu wa kusaidia usajili pamoja na kuongeza mikataba kwa nyota mbalimbali kila inapohitajika.

Mpanzu alisaini mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru Disemba 2024 na sasa ameongeza mingine miwili.

Mpanzu anakuwa mchezaji watatu kuongeza mkataba mpya kuelekea msimu mpya wa mashindano 2026/2027 kutokana na ubora aliounyesha mpaka sasa.

Advertisement

Benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker limeidhinisha kuongezwa kwa mkataba wa nyota huyo raia wa DR Congo na Mo amekamilisha suala hilo.

Nyota wengine ambao tayari wameongezwa mkataba kuelekea msimu mpya wa mashindano ni mlinzi wa kati, Rushine De Reuck na kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma.

Back to homepage
Share this story