Simba Sports Club
News

Mo akutana na benchi la Ufundi na Wachezaji

7 Jul 2024

Mo amesema ana matumaini makubwa na kikosi kilichosajiliwa pamoja na benchi la ufundi lililopo.

Mo ameweka wazi kuwa malengo yake ni kuiona Simba inachukua ubingwa wa Afrika na hilo linatakiwa kuwa kwenye vichwa vya wachezaji na siku zote wanatakiwa kujua hilo.

Pamoja na hilo Mo amewasisitiza wachezaji na benchi la ufundi lengo mama kwa sasa ni kuhakikisha tunarejesha mataji yote tuliyopoteza katika miaka ya karibuni.

Advertisement

"Mimi pamoja na Bodi nzima ya Wakurugenzi tunawaamini nyinyi wote, na kila mmoja anatakiwa kufahamu Simba ni timu kubwa na ina mahitaji makubwa pia kwahiyo anatakiwa ajitume ili kufanikisha malengo ya timu."

"Siku ya kwanza wakati nimekuja kuwekeza katika klabu hii malengo yangu niliweka wazi kabisa kuwa ni kuiona Simba inachukua ubingwa wa Afrika hilo likitimia nafsi yangu itatulia na litawezekana kama wachezaji mtajitoa hadi mwisho kwenye kila mchezo," amesema Mo.

Back to homepage
Share this story