Mo ameungana na Watanzania wengine ambao wamenunua tiketi kwa ajili ya kutoa hamasa kwa Taifa Stars ili kupata ushindi kesho na hatimaye tujiweke katika nafasi ya kufuzu fainali hizo.
Wadhamini wetu Africarriers nao wamenunua tiketi 2000 kuchangia hamasa kuelekea mchezo wa kesho kwakuwa hili ni suala la kitaifa.
Advertisement
Juzi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' nae amechangia tiketi 500 huku Mwenyekiti wa klabu Murtaza Mangungu nae akichangia tiketi 600.