Mlinzi wa kati Jordan Adeoti wa timu ya Taifa ya Benin amemmwagia sifa kiungo wetu Mzamiru Yassin kutokana na kiwango alichoonyesha kwenye mchezo wa jana wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kati ya Tanzania na Benin na kusema anaweza kucheza soka barani Ulaya.
Baada ya mchezo kumalizika, Adeoti anayekipiga Klabu ya Annecy ya Ufaransa alimfuata Mzamiru na kumpongeza na kumuuliza anacheza timu gani.
Mzamiru amesema Adeoti amemuuliza kwanini bado anacheza ligi ya ndani wakati ana uwezo wa kukipiga barani Ulaya kutokana na uwezo wake.
"Ameniuliza kwanini bado anacheza ligi ya ndani wakati nina uwezo wa kucheza hata Ulaya, kiukweli maneno yake yamenipa sababu ya kuendelea kupambana," amesema Mzamiru.
Mzamiru ataukosa mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili nchini Benin kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.