Simba Sports Club
News

Mligo awasili kambini Misri

8 Aug 2025

Mligo tumemsajili Jumanne ya wiki hii kutoka Namungo FC kwa mkataba wa miaka mitatu na baada ya kukamilisha taratibu zote tayari amejiunga na wenzake kambini.

Mligo amewasili kambini mchana wa leo na amefanya mazoezi ya Gym kuweka mwili sawa ambapo kuanzia kesho ataendelea na programu ya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake.

Advertisement

Ukitoa wachezaji wanaoshiriki michuano ya CHAN, Mligo ndiye pekee ambaye alikuwa bado hajajiunga na timu kambini lakini wengine wote wanaendelea na maandalizi.

Back to homepage
Share this story