Simba Sports Club
News

Mkude, Kibu kuikosa Mtibwa Jumamosi

20 Jan 2022

Kiungo mkabaji Jonas Mkude na mshambuliaji Kibu Denis hawatakuwa sehemu ya kikosi kinachosafiri kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumamosi kutokana na kuwa na majeruhi.

Wawili hao walipata maumivu katika mechi yetu iliyopita dhidi ya Mbeya City ambapo walishindwa kuendelea na mchezo kipindi cha pili.

Advertisement

Hata hivyo, nyota hao wanaendelea vizuri na wamepumzishwa ili hali zao zirejee katika utimamu na wanatarajia kuwepo katika mchezo utakaofuata.

Mkude na Kibu wanaungana na Thadeo Lwanga ambaye ni majeruhi wa muda mrefu lakini anatarajia kurudi uwanjani kabla ya mwezi huu kumalizika.

Back to homepage
Share this story