Nyota watatu wameingia kwenye fainali ya kinyang'anyiro cha kuwania mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Wachezaji walioingia fainali kutokana na uwezo walioonyesha ni kiungo mkabaji Jonas Mkude, walinzi wakati Henock Inonga na Joash Onyango.
Katika mwezi Desemba, Mkude amecheza mechi nne kati ya tano ambazo amecheza dakika zote 90 huku akisaidia kupatikana kwa mabao mawili (assist) wakati Onyango na Henock wakicheza mechi tatu kila mmoja kwa kiwango cha juu.
Awali walikuwa wachezaji watano pamoja na Kibu Denis na Sadio Kanoute lakini wawili hao wamechujwa na Kamati Maalum ya tuzo na kuwabakisha Mkude, Onyango na Henock.
Zoezi la mashabiki kupiga kura limeanza leo kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Januari mosi saa 10 jioni ambapo mwenye kura nyingi atatangazwa mshindi.
Mshindi atakabidhiwa tuzo na pesa taslimu Sh. 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP kama sehemu ya zawadi.
[totalpoll id="6832"]